Sudan Kusini yalenga kutoa chanjo ya surua kwa watoto milioni 3.4

(CRI Online) Februari 14, 2025

Sudan Kusini kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, imezindua kampeni ya nne ya chanjo ya surua jana jumatano, ikiwa na lengo la kutoa chanjo kwa watoto milioni 3.47 wenye umri wa kati ya miaka 0 mpaka mitano.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Harriet Paquale amesema, chanjo hiyo inalenga kuondoa maambukizi ya virusi vya surua kwa watoto nchini humo.

Kampeni hiyo inayoongozwa na Wizara ya Afya ya Sudan Kusini ikiungwa mkono na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), inafuatia kuthibitishwa kwa matukio 36 ya virusi vya surua katika kaunti nane nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha