

Lugha Nyingine
Rais wa China atoa salamu za pongezi kwa Mkutano wa kilele wa 38 wa AU
(CRI Online) Februari 17, 2025
Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa njia ya simu kwa Mkutano wa kilele wa 38 wa Umoja wa Afrika (AU).
Katika salamu hizo, Rais Xi amezitakia nchi na watu wa Afrika mafanikio mapya na makubwa katika njia yao ya kujiendeleza na kupata ustawi.
Pia amesisitiza kuwa China iko tayari kushirikiana na viongozi wa nchi za Afrika, kuhimiza utekelezaji wa mapendekezo sita na mpango wa “Hatua 10 za Ushirikiano” za kuhimiza mchakato wa mambo ya kisasa, ili kunufaisha watu zaidi ya bilioni 2.8 wa China na Afrika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma