

Lugha Nyingine
Idadi ya watu waliofariki kufuatia kuporomoka kwa mgodi haramu wa dhahabu nchini Mali yafikia 50
(CRI Online) Februari 17, 2025
Idadi ya watu waliofariki kufuatia ajali ya kuporomoka kwa mgodi haramu wa dhahabu huko Kenieba, Kayes, nchini Mali, Jumamosi mwishoni mwa wiki imefikia 50.
Ajali hiyo imesababishwa na mashine iliyoanguka kwenye mgodi wa madini, ambapo kundi la watu walikuwa wakichimba dhahabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka husika, kwa sasa kazi ya uokoaji imekamilika na hakuna watu waliopatikana kutoka kwenye vifusi vya mgodi huo.
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Mali Abdoulaye Maiga jana usiku amesema, serikali itachukua hatua "kali zaidi" dhidi ya ajali za mgodini.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma