

Lugha Nyingine
Afrika yapata maendeleo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria
Maofisa na wataalamu wa Afrika wametoa wito kuendelea kulisaidia bara hilo katika mapambano dhidi ya malaria, wakionya kuwa maendeleo yaliyopatikana katika kupambana na ugonjwa huo barani Afrika yako hatarini kutokana na changamoto za kiasili na zinazosababishwa na binadamu.
Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Malaria uliofanyika jana Jumapili pembezoni mwa Mkutano wa Kilele wa 38 wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais wa Botswana Duma Boko amesisitiza kwamba maendeleo chanya ya Afrika katika kupambana dhidi ya malaria yameathiriwa na sababu kadhaa, ikiwemo uhaba wa fedha, na majanga ya kiasili na kibinadamu.
Naye kaimu mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika Chikwe Ihekweazu amesema, nchi za Afrika zimeendelea kukabiliwa na changamoto zinazokwamisha kutokomeza kabisa ugonjwa huo wa malaria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma