

Lugha Nyingine
Serikali ya DRC yathibitisha waasi wa M23 kuingia Bukavu
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imelaani vikali kitendo cha waasi wa kundi la M23 kuingia katika mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kusini, wa Bukavu, na kushikilia maeneo muhimu ya kimkakati katika mji huo.
Katika taarifa yake, serikali ya DRC imeuhakikishia umma kwamba inafuatilia kwa karibu hali ya Bukavu, ambako waasi wa M23 waliingia jana Jumapili asubuhi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchini humo, waasi hao wa M23 walithibiti maeneo mengi ya kimkakati mjini humo siku ya Jumamosi asubuhi, ikiwemo makazi ya gavana wa Jimbo la Kivu Kusini.
Serikali imesisitiza tena ahadi yake ya kurejesha utaratibu, usalama na mamlaka halali ya ardhi, na kuwataka wakazi wa Bukavu kutotoka nje ili kuepuka kulengwa na waasi hao.
Mapema siku hiyo ya Jumapili, Ikulu ya DRC ilitoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba mji wa Bukavu ambao ulikaliwa na waasi wa M23, ulikuwa uko chini ya jeshi la nchi hiyo na washirika wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma