China yaitaka Marekani kusahihisha makosa ya maneno kuhusu Taiwan kwenye tovuti ya Wizara yake ya Mambo ya Nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2025

BEIJING – Kile kinachoitwa "mapitio" kwenye nyaraka ya ukweli wa Taiwan inayoonyeshwa kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ni mfano mwingine wa Marekani kulitumia suala la Taiwan kuizuia China, na China inaitaka Marekani kusahihisha mara moja makosa yake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema Jumatatu.

Awali iliripotiwa kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imefanya "mapitio" kwenye nyaraka ya ukweli wa Taiwan inayoonyeshwa kwenye tovuti yake, ambayo imeondoa maneno yake ya awali ambayo yalikuwa yasema haiungi mkono Taiwan kujitenga na China.

Guo amesisitiza kwamba kuna China moja tu na Taiwan ni sehemu ya China, na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo serikali pekee halali kisheria inayowakilisha China nzima, akiongeza kuwa ni makubaliano ya kimataifa yaliyopo na kanuni za kawaida zinazoongoza uhusiano wa kimataifa, na pia ni ahadi inayotolewa na Marekani katika taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani.

Guo amesisitiza kuwa marekebisho hayo yaliyofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwenye nyaraka yake hiyo ya ukweli wa Taiwan yamerudisha nyuma sana msimamo wake kuhusu masuala yanayohusiana na Taiwan, na yametuma ishara mbaya sana kwa vikundi vinavyotaka "Taiwan Ijitenge".

"Tunaitaka Marekani kurekebisha mara moja makosa yake, kuheshimu kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani," Guo amesema, akiitaka Marekani kuacha kupandisha hadhi uhusiano halisi na Taiwan, kujizuia kuunga mkono Taiwan katika kupanua nafasi yake ya kimataifa, na kuacha kuhamasisha na kuunga mkono "Taiwan Ijitenge" na kuepuka uharibifu mkubwa zaidi kwenye uhusiano kati ya China na Marekani na amani na utulivu kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha