Kamati ya Kudumu ya Bunge la China yapanga mkutano wake kufanyika mwishoni mwa Februari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2025

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akiongoza mkutano wa 38 wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, China, Februari 17, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akiongoza mkutano wa 38 wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Februari 17, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China itafanya mkutano wake wa 14 mjini Beijing Februari 24 na 25. Uamuzi huo umefanywa jana Jumatatu kwenye mkutano wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge hilo, ambao uliongozwa na Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge hilo.

Kwa mujibu wa ajenda iliyojadiliwa kwenye kikao hicho, kazi muhimu ya mkutano huo ujao itakuwa kuandaa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, utakaofanyika mwezi Machi.

Wajumbe kwenye mkutano huo wa mwishoni mwa Februari watajadili ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge hilo, mswada wa ajenda ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14, mswada wa orodha ya majina ya watu wa Tume ya Utendaji wa Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 na katibu mkuu wa tume hiyo, pamoja na mswada wa orodha ya majina ya wajumbe wasikilizaji wa mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano huo ujao pia watapitia mswada wa sheria ya kuhimiza uchumi binafsi, pendekezo lililowasilishwa na Baraza la Serikali la China juu ya kuthibitisha mswada wa marekebisho ya sheria ya usafiri wa anga, ripoti kuhusu hali ya baadhi ya wajumbe wa Bunge la Umma, vilevile mswada husika wa uajiri.

Kwenye mkutano huo wa Jumatatu pia imejadiliwa miswada ya njia za kufanya rekodi na ukaguzi wa mambo ya bajeti ya fedha, pamoja na ripoti ya ofisi za Bunge la Umma la China kuhusu kushughulikia malalamiko ya umma katika mwaka 2024. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha