“Ne Zha 2” yaingia katika filamu kumi za wakati wote kwa mapato makubwa zaidi ya tiketi duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2025

Watu wakitazama filamu ya “Ne Zha 2” kwa muundo wa 4D kwenye ukumbi wa sinema mjini Beijing, Februari 16, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Watu wakitazama filamu ya “Ne Zha 2” kwa muundo wa 4D kwenye ukumbi wa sinema mjini Beijing, Februari 16, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Kwa mujibu wa takwimu za jukwaa la mauzo ya tiketi mtandaoni la Maoyan, hadi kufikia mchana wa jana Jumatatu, filamu maarufu ya katuni ya China “Ne Zha 2” ilikuwa imeipita filamu ya Disney “The Lion King” ya mwaka 2019 kuchukua nafasi ya kuwa miongoni mwa filamu 10 za wakati wote duniani kwa mapato makubwa ya mauzo ya tiketi za kuitazama, ikiwa na mapato ya duniani, yakiwemo mauzo ya tiketi za kabla, yanayozidi Yuan bilioni 12.05 (karibia dola za Marekani bilioni 1.67).

Mafanikio hayo yamekuja ikiwa ni siku ya 20 tangu filamu hiyo kutolewa kwa mara ya kwanza kutazamwa na umma wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China Januari 29.

Yanaongeza katika orodha inayoongezeka ya rekodi zilizowekwa na filamu hiyo, ambayo imekuwa filamu ya kwanza kuingiza dola za Marekani bilioni 1 katika soko moja na filamu ya kwanza isiyo ya Hollywood kuingia klabu ya mapato ya dola-bilioni.

Watu wakiangalia bango la filamu ya “Ne Zha 2” kwenye ukumbi wa sinema mjini Beijing, China, Februari 16, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Watu wakiangalia bango la filamu ya “Ne Zha 2” kwenye ukumbi wa sinema mjini Beijing, China, Februari 16, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha