China yampongeza Bw. Mahmoud Youssouf kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika

(CRI Online) Februari 18, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Guo Jiakun amempongeza Bw. Bw. Mahmoud Youssouf kwa kuchaguliwa na Mkutano wa 38 wa Umoja wa Afrika kuwa mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kipindi cha miaka minne.

Bw. Youssouf Youssouf ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti kabla ya kuchaguliwa kwake, amechaguliwa kwenye mkutano huo uliofikia tamati mwishoni mwa wiki, siku ya Jumapili.

Katika pongezi hizo zilizotolewa jana Jumatatu, Msemaji Guo amesisitiza kuwa, China iko tayari kushirikiana naye kwa karibu na Kamisheni ya awamu mpya ya Umoja wa Afrika, kuendelea kuunga mkono kazi ya uongozi wa Umoja huo katika mchakato wa ujumuishaji wa Afrika, kutoa sauti yenye nguvu zaidi katika mambo ya kikanda na kimataifa, na kushirikiana na Umoja wa Afrika kuhimiza kwa pamoja uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Amesema uhusiano kati ya China na Afrika unaendelea kupata maendeleo ya kina, na kuongoza Nchi za Kusini kujiimarisha na kuhimiza kwa ushirikiano mchakato wa mambo ya kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha