Jeshi la Sudan lapata maendeleo makubwa ya kijeshi katika eneo la mji mkuu

(CRI Online) Februari 18, 2025

Jeshi la Sudan limesema vikosi vyake vimepata maendeleo makubwa katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) katika maeneo mbalimbali.

Jeshi hilo limesema katika taarifa yake kwamba, katika mapambano mjini Bahr, kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, jeshi hilo limefanikiwa kukomboa kikamilifu eneo la Kafouri, ambalo ni ngome kuu ya mwisho ya Kikosi RSF katika mji huo.

Jeshi la Sudan limesema, limefanikiwa kuwafukuza wapiganaji wa RSF kutoka eneo la Kafouri na kurejesha udhibiti wa makao makuu ya viwanda vya mfumo wa ulinzi wa taifa.

Jeshi la Sudan pia limetoa taarifa nyingine jana Jumatatu likisema kuwa limeudhibiti mji wa al-Rahad katika Jimbo la Kordofan, kaskazini, magharibi mwa nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha