Mkutano wa mambo ya mazingira watoa njia ya mageuzi ya kijani barani Afrika

(CRI Online) Februari 18, 2025

Mkutano wa The Green and Resilient UrbanShift Africa 2025 uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, umetoa wito kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na malengo ya kimkakati, uongozi unaotazama siku zijazo, na sera mpya ili kuendeleza mageuzi ya kijani na maendeleo ya miji.

Mkutano huo uliofanyika jana Jumatatu umewakutanisha wajumbe zaidi ya 250, wakiwemo wakuu wa miji, wabunge, wawekezaji, watetezi wa mazingira na wavumbuzi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Freetown nchini Sierra Leone, Yvonne Aki-Sawyerr amesema miji ya barani Afrika imetoa kipaumbele katika hatua za mwitikio wa mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia uvumbuzi unaoongozwa na vijana.

Gavana wa Jiji la Nairobi Johnson Sakaja amesema, inawezekana kwa Afrika kubadili miji yake kuwa maeneo ya kuvutia yanayoweza kuvutia uwekezaji katika suluhu zinazotokana na watu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kama nishati safi na usafiri.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha