

Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika watoa wito kwa waasi wa M23 kuondoka mara moja nchini DRC
(CRI Online) Februari 18, 2025
Viongozi wa Afrika waliokuwa wakihudhuria Mkutano wa 38 wa Viongozi Wakuu wa Umoja wa Afrika wamelitaka kundi la waasi wa M23 kuondoka mara moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika mkutano na wanahabari uliofanyika kando ya Mkutano huo mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Kamishna wa Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika Bankole Adeoye amesema, viongozi wa Afrika wametoa wito wa kulinda na kuheshimu uhuru, umoja wa kisiasa na ukamilifu wa ardhi ya DRC.
Amesema Umoja wa Afrika unafuatilia kwa karibu mgogoro huo na kupendekeza kuongeza kasi ya utekelezaji wenye ufanisi wa makubaliano ya Luanda na Nairobi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma