Wataalamu wa Umoja wa Mataifa watembelea Sudan Kusini kufuatilia hali ya haki za binadamu

(CRI Online) Februari 18, 2025

Wataalamu huru wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wameanza ziara ya siku nne nchini humo kuanzia jana Jumatatu kujadili hali ya haki za binadamu nchini humo.

Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo Yasmin Sooka amesema, wataalamu hao watakutana na maofisa wa serikali, wahanga wa ukiukaji wa haki za binadamu, wajumbe wa mashirika ya kiraia, wanasheria, na wawakilishi wa jumbe za kidiplomasia na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Kamisheni hiyo inatarajiwa kuwasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa mataifa mjini Geneva wiki ijayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha