

Lugha Nyingine
Mkutano wa Kilele wa AU wapaza wito wa pamoja wa nchi za Kusini zinazoibukia
Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2025 ikionyesha majengo ya Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)
ADDIS ABABA - Viongozi wa nchi za Afrika walikusanyika mjini Addis Ababa Ethipia kuanzia Jumatano hadi Jumapili kuhudhuria mkutano wa kilele wa mwaka wa AU, wakijikita katika harakati za bara hilo za kujitegemea, juhudi za kurekebisha dhuluma za kihistoria, na upigaji hatua thabiti kuelekea malengo ya mambo kisasa yaliyowekwa katika Ajenda ya 2063.
Huku Nchi za Kusini zikiibuka kama nguvu kubwa katika kuunda upya utaratibu wa dunia, Mkutano wa 38 wa Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika chini ya kaulimbiu ya "Haki kwa Waafrika na Watu Wenye Asili ya Afrika Kupitia Fidia," umepaza wito wa pamoja wa kundi hilo wa haki na usawa ndani ya mfumo wa usimamizi wa kimataifa.
Kurekebisha makosa ya kihistoria
Ujenzi wa mambo ya kisasa ni haki isiyoepukika ya nchi zote. Hata hivyo nchi za Magharibi zilitafuta ujenzi wake wa mambo ya kisasa kwa gharama ya nchi nyingi zinazoendelea. Ukoloni, biashara ya watumwa iliyovuka Bahari ya Atlantiki, ubaguzi wa rangi kimatabaka, na ubaguzi wa rangi wa kimfumo uliliathiri vibaya Bara la Afrika, huku ardhi iliyokuwa ikistawi ikipunguzwa kuwa wasambazaji tu wa malighafi na maeneo ya kutupa bidhaa za Magharibi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia wakuu wa nchi na serikali za Afrika kwenye mkutano huo kwamba bara hilo lilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wakati mfumo wa sasa wa pande nyingi ulipokuwa ukiundwa, na kwamba ukosefu wa haki unadumu.
Hata hivyo, kufuatia kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, Nchi za Dunia ya Tatu, zikiwemo nchi za Afrika, zilipata uhuru na kuanza mchakato wa maendeleo, kurekebisha kila mara dhuluma hizo za kihistoria katika safari nzima ya mchakato wao wa ujenzi wa mambo ya kisasa.
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete (wa kwanza kulia) akihutubia Mkutano wa 46 wa Kawaida wa Baraza Tendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 12, 2025. (Xinhua/Michael Tewelde)
Kwenye mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete alisisitiza kuwa Afrika imekuwa ikikabiliwa na vizuizi vya kimuundo vya muda mrefu ambavyo vinaweka nchi katika bara hilo kwenye mzunguko wa utegemezi wa kiuchumi.
Ametoa wito wa mageuzi ya muundo wa mfumo wa mambo ya fedha duniani, urekebishaji wa madeni, kuanzisha wakala wa ukadiriaji viwango vya mikopo unaoongozwa na Afrika, kuhimiza Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, na kuweka kipaumbele katika uongezaji thamani ndani ya bara hilo.
Kujikita katika uhuru, kujitegemea
Katika njia kuelekea kujitegemea na maendeleo, AU pia imegeuza mkazo wake kwa ndani, ikiwezesha maendeleo kwa kuamsha ustawi wa bara lenyewe.
Kwenye mkutano huo, viongozi wa Afrika walishiriki katika majadiliano kuhusu kuondoleana viza, Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA), na kuanzishwa kwa Wakala wa Ukadiriaji Viwango vya Mikopo wa Afrika.
Viongozi wa Afrika kwa muda mrefu wamekuwa wakifikiria siku zijazo ambapo biashara haitakuwa ukizuiliwa tena na mipaka ya kijiografia. Kwa mfano, raia wa Ivory Coast anaweza kuagiza kwa urahisi nguo zilizobuniwa Msumbiji mtandaoni kwa kubofya mara moja tu, na magari yaliyotengenezwa Afrika Kusini yanakuwa na bei nafuu zaidi kuliko ya kutoka Ulaya. Kuanzishwa kwa AfCFTA ni hatua muhimu katika kugeuza matumaini hayo kuwa uhalisia.
Hadi sasa, nchi 47 kati ya nchi wanachama 55 wa AU zimeridhia mkataba huo wa AfCFTA. Biashara isiyo na ushuru kati ya nchi za Afrika inapanuka, huku usambazaji huria wa bidhaa ukionekana kuwa halisi zaidi na wenye ushawishi mkubwa.
Mwanamume akiwa ameketi nje ya jengo la ofisi ya Sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) mjini Accra, mji mkuu wa Ghana, Agosti 17, 2020. (Ikulu ya Ghana/ kupitia Xinhua)
Benki ya Dunia ilikadiria kuwa mkataba huo wa biashara huria unaweza kuondoa watu milioni 30 kutoka kwenye umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2035, kuongeza mapato ya kikanda kwa dola za Kimarekani bilioni 450, na kuongeza mauzo ya nje kati ya bara kwa asilimia 81.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma