

Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan yasema raia 433 wameuawa katika mashambulizi ya kikosi cha RSF
(CRI Online) Februari 19, 2025
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema, katika siku kadhaa zilizopita, raia 433 wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo wa Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) dhidi ya vijiji vingi katika Jimbo la White Nile, katikati mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Wizara hiyo imesema, kitendo cha kikosi hicho ni cha kulipiza kisasi kwa kuua raia baada ya kushindwa kupambana na Jeshi la Sudan, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kukilaani vikali kitendo hicho.
Mpaka sasa, kikosi hicho cha RSF hakijatoa kauli yoyote kuhusu mashambulizi hayo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma