

Lugha Nyingine
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki yatafuta fedha na ushirikiano wa nguvu zaidi wa kimahakama
Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa wito wa kuongeza kidhahiri bajeti yake na ushirikiano wa kina zaidi wa kimahakama ili kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tatu wa Mwaka wa Mahakama hiyo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza Jumatatu wiki hii mjini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, na unatazamiwa kumalizika tarehe 8 mwezi ujao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Mahakama hiyo Nestor Kayobera ameshukuru nia njema ya nchi wanachama katika utekelezaji wa maamuzi ya mahakama lakini amesisitiza kuwa uhaba wa fedha unakwamisha utendaji wa mahakama hiyo.
Licha ya rasilimali ya fedha, Kayobera ametoa wito wa ushirikiano zaidi wa kimahakama katika kanda hiyo, na kusisitiza haja ya ushirikiano wa karibu kati ya mahakama za kitaifa na EACJ ili kuhakikisha matumizi endelevu ya sheria na utekelezaji wa ufanisi wa maamuzi ya mahakama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma