Ethiopia yapongeza maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika kujitosheleza kwa chakula

(CRI Online) Februari 19, 2025

Serikali ya Ethiopia imepongeza mafanikio ya nchi hiyo katika uzalishaji wa ngano, kama sehemu ya lengo la kitaifa la kutimiza kujitosheleza kwa chakula.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Jumanne, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia imesema nchi hiyo imezalisha tani milioni 23 za ngano katika msimu wa mavuno wa mwaka 2023/2024.

Ofisi hiyo imesema, awali Ethiopia ilikuwa ikitumia dola za kimarekani karibu bilioni moja kila mwaka kununua ngano ili kukabiliana na mahitaji ya nchi hiyo kutokana na uzalishaji hafifu, na kuongeza kuwa, tangu msimu wa mavuno wa mwaka 2020/2021, nchi hiyo iliacha kuagiza ngano kutoka nje.

Serikali ya Ethiopia imesema Mkakati huo wa kuongeza uzalishaji wa ngano umeibadili nchi hiyo kutoka kuwa mwagizaji wa ngano hadi mzalishaji anayejitegemea, ikionyesha mafanikio katika sera zake za kilimo, miradi na mapendekezo husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha