EAC yapanga kuanzisha taasisi ya vyanzo vya asili vya nishati

(CRI Online) Februari 19, 2025

Baraza la Nishati, Mafuta na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) limekubali kuanzisha taasisi itakayosimamia vyanzo vya asili vya nishati na ufanisi wa nishati.

Taarifa ya Jumuiya hiyo iliyotolewa jana Jumanne imesema, uamuzi huo umefikiwa kwenye Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri wa Nishati wa EAC uliofanyika katika makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha, Tanzania.

Taarifa hiyo imesema, majukumu ya jumla ya taasisi hiyo ni kuhamasisha nchi wanachama wa EAC kutoa utaratibu, ambapo sekta binafsi na washirika wa maendeleo wanaweza kuchukua nafasi kubwa katika kuzisaidia nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuondoa uhaba wa upatikanaji wa nishati, kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya nishati, na kuchangia katika mwitikio wa mabadiliko ya tabianchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha