

Lugha Nyingine
China yatoa wito wa mfumo wa kweli wa pande nyingi, mfumo wa usimamizi wa dunia wenye usawa zaidi
UMOJA WA MATAIFA - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa hotuba Jumanne kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu "Kutekeleza Mfumo wa Pande Nyingi, Kuufanyia Mageuzi na Kuboresha Usimamizi wa Dunia" akitoa wito wa kuhimiza mfumo wa kweli wa pande nyingi na kuharakisha juhudi za kujenga mfumo wa usimamizi wa Dunia ulio wa haki na usawa zaidi.
Mwaka 2025 ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, Wang amesema, akiongeza kuwa historia hiyo ya miaka 80 ni ufunuo wa maarifa vya kutosha na kwamba katika kukabiliana na misukosuko na mabadiliko ya mazingira ya kimataifa, mfumo wa kimataifa unaozingatia Umoja wa Mataifa unatoa uhakikisho muhimu kwa harakati za upigaji hatua wa binadamu, na kwamba mfumo wa pande nyingi juu ya msingi wa uratibu na ushirikiano ni suluhisho bora zaidi kwa masuala ya kimataifa.
"Katika kukabiliana na mwenendo wa kihistoria wa mustakabali wa pamoja, hakuna nchi inayoweza kustawi peke yake, na ushirikiano wa kunufaishana ni chaguo sahihi," Wang amesema, akiongeza kuwa katika kukabiliana na mabadiliko makubwa ya mazingira ya kimataifa, Nchi za Kusini hazipaswi tu kufikia hatua ya kihistoria ya kusonga mbele pamoja kuelekea mambo ya kisasa, lakini pia kubaki mstari wa mbele katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia.
"Katika zama ambazo misukosuko na mageuzi yanaongezeka, tunahitaji, zaidi ya hapo awali, kujikumbusha juu ya dhamira ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, kuimarisha upya mfumo wa kweli wa pande nyingi, na kuharakisha juhudi za kujenga mfumo wa usimamizi wa kimataifa wenye haki na usawa," amesema Wang.
Kuhusiana na hili, Wang ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ametoa pendekezo lenye vipengele vinne: Kwanza, kushikilia usawa wa mamlaka za nchi, pili, kushikilia haki na usawa, tatu, kushikilia mshikamano na uratibu na nne, kushikilia mbinu yenye mwelekeo wa vitendo.
Kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, Wang amesema ni muhimu kushikilia suluhu ya nchi mbili, kusukuma utatuzi wa pande zote, wenye haki na wa kudumu wa suala la Palestina, na kuleta amani na usalama wa kudumu katika Mashariki ya Kati.
Kuhusu mgogoro wa Ukraine, Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa China amesema tangu kuanza kwa mgogoro huo, China imekuwa ikitoa wito wa suluhu ya kisiasa na kusukuma mazungumzo ya amani, na kwamba China inaunga mkono juhudi zote zinazoleta amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma