China yatoa mpango wa utekelezaji wa kutuliza uwekezaji wa kigeni katika mwaka 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2025

BEIJING –China imetoa mpango wa utekelezaji wa kuleta utulivu kwenye uwekezaji wa kigeni katika mwaka 2025, ambao umeidhinishwa kwenye mkutano wa utendaji wa Baraza la Serikali la China hivi karibuni.

Mpango huo umeandaliwa na Wizara ya Biashara ya China na Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, taarifa iliyotolewa na Ofisi Kuu ya Baraza la Serikali la China imeeleza.

Uwekezaji wa kigeni ni kipengele muhimu cha kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na una mchango muhimu katika kujenga na kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuendeleza mambo ya kisasa ya China, kwa mujibu wa mpango huo, ambao umeandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha uwekezaji tulivu wa kigeni katika mwaka 2025.

Kwa mujibu wa mpango huo, China itaunga mkono maeneo ya majaribio katika kutekeleza ipasavyo sera za ufunguaji mlango zinazohusiana na maeneo kama vile mawasiliano ya simu ya ongezeko la thamani, teknolojia za mambo ya tiba na hospitali zinazomilikiwa na wawekezaji wa kigeni kabisa, ikitoa huduma za safari nzima kwa miradi iliyowekezwa na wageni katika sekta hizo.

Mpango huo unasema, China itatumia mpango huo kufungua zaidi sekta ya elimu na utamaduni, kuchapisha mipango ya utekelezaji na kusukuma mbele mipango hiyo kwa kasi.

Mpango kazi huo unatoa wito wa juhudi za kupanua mpango wa kitaifa wa majaribio ili kufungua sekta ya huduma zaidi na kuhimiza ufunguaji mlango wenye utaratibu wa sekta ya matibabu.

Aidha, unasisitiza kuhimiza uwekezaji wa hisa za kigeni nchini China ili kuvutia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja wenye ubora wa hali ya juu katika kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa nchini humo.

“China itaondoa vikwazo kwa kampuni za kigeni kupata mikopo nchini China, kuruhusu kampuni hizo kutumia fedha za ndani kwa uwekezaji wa usawa,” mpango huo unaeleza.

Unaangazia sekta muhimu ili kuvutia uwekezaji wa kigeni. Kwa mujibu wa mpango huo, kampuni za kigeni zinahimizwa kuwekeza katika sekta zinazohusiana na ufugaji kama vile uzalishaji mifugo, utengenezaji wa vifaa vya kulisha mifugo na utengenezaji wa malisho na dawa za mifugo, na kufurahia huduma ya kitaifa.

Pia unaunga mkono kampuni za kigeni kushiriki katika maendeleo mapya ya viwanda ya China, kwa kujikita zaidi katika nyanja za teknolojia ya hali ya juu. Uwekezaji wa kigeni pia unakaribishwa katika sekta za huduma kama vile huduma kwa wazee, utamaduni na utalii, michezo, huduma za afya, elimu ya ufundi stadi, na mambo ya fedha.

Mwaka 2024, kampuni mpya 59,080 zilizowekezwa kwa mtaji wa kigeni zilianzishwa nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.9 mwaka hadi mwaka. China ilivutia uwekezaji wa mwaka wa nje wenye thamani ya yuan zaidi ya trilioni 1 (dola za kimarekani karibu bilioni 139.5) kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2021 hadi 2023.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha