Wataalamu wa China wang’ara katika maonyesho ya kilimo nchini Cote d’Ivoire

(CRI Online) Februari 20, 2025

China imeng'ara katika uzinduzi wa Maonyesho ya kwanza ya Kimataifa ya Rasilimali ya Kilimo na Mifugo ya Abidjan Mwaka 2025 (SARA), yanayolenga mifumo ya mchakato wa kilimo na chakula ili kutimiza usalama wa chakula na mapinduzi ya kilimo barani Afrika.

Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Robert Mambe amesema kwenye uzinduzi wa maonyesho hayo, kwamba ni fahari kuwa na washiriki kutoka China, nchi ambayo utaalamu wake wa kilimo ni mfano wa kuigwa.

Amesema China ni mgeni wa heshima katika maonyesho hayo ya mwaka huu kutokana na uongozi wake katika uzalishaji wa kilimo duniani na ubora wake wa uhusiano wa ushirikiano na Cote d'Ivoire.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha