Watu 53 wafariki kutokana na ugonjwa usiojulikana nchini DRC

(CRI Online) Februari 20, 2025

Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni limesema, watu 53 wamefariki na wengine 431 kuambukizwa virusi vya ugonjwa usiojulikana katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na WHO, ugonjwa huo umetokea katika Jimbo la Equateur nchini humo, na mamlaka za afya za eneo hilo ziligundua ugonjwa huo katika vijiji viwili vya jimbo hilo mwezi Januari na Februari mwaka huu.

Dalili za mgonjwa ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, na kuhara, huku baadhi ya wagonjwa wakitokwa na damu puani na kutapika damu.

WHO limesema ugonjwa huo hauhusiani na virusi vya Ebola na Marburg, na kwamba mamlaka za afya nchini DRC zinaendelea kufanya uchunguzi kuhusu ugonjwa huo.

Chanzo:cri

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha