Umoja wa Mataifa wapanga kufungua ofisi 3 mpya nchini Kenya

(CRI Online) Februari 20, 2025

Umoja wa Mataifa unapanga kufungua ofisi tatu mpya za kimataifa nchini Kenya hadi kufikia mwisho wa mwaka 2026, ikiimarisha majukumu ya Nairobi, mji mkuu wa nchi hiyo, kama kitovu muhimu kwa shughuli za Umoja huo.

Mkuu wa Mawaziri wa Kenye ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora Musalia Mudavadi amesema hayo baada ya kufanya mkutano na mwenyekiti wa Baraza Kuu la 79 la Umoja wa Mataifa Philemon Yang, ambaye yuko ziarani nchini Kenya.

Mudavadi amesema ofisi hizo tatu mpya zitahudumia Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu Duniani, na Taasisi ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake ya Umoja huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha