

Lugha Nyingine
Kituo cha mafunzo ya lugha ya Kichina chazinduliwa nchini Ghana
Kituo cha Elimu na Ushirikiano wa Lugha (CLEC) na Kituo Kikuu cha Cape Coast (UCC) nchini Ghana Jumatano zimeanzisha kituo cha mafunzo kwa walimu wa lugha ya Kichina katika kanda ya Afrika Magharibi.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo hicho, Makamu wa rais wa UCC Bw. Denis Aheto amesema, kuanzishwa kwa kituo hicho kunawakilisha hatua kubwa na muhimu katika kuunganisha tamaduni, kuimarisha ushirikiano wa elimu na kuwapa walimu wenyeji ujuzi muhimu wa kufundisha lugha ya Kichina kwa njia yenye ufanisi.
Naye Naibu mkurugenzi wa CLEC Bw. Hu Zhiping amesema, mahitaji ya kujifunza lugha ya Kichina barani Afrika yamekuwa yakiongezeka katika miaka ya karibuni, na kwamba uzinduzi wa kituo hicho unalenga kutoa mafunzo kwa walimu zaidi wa lugha ya Kichina, na kuhimiza maendeleo endelevu ya lugha ya Kichina katika kanda hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma