

Lugha Nyingine
Sudan yamwita nyumbani balozi wake nchini Kenya
Ripoti iliyotolewa na Shirika la Habari la Sudan SUNA imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imemwita nyumbani Balozi wake nchini Kenya Kamal Jubara, ikiwa ni sehemu ya kupinga hatua ya Kenya kuwa mwenyeji wa mkutano uliohusisha Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) na washirika wake wa kisiasa.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, kilichotokea Nairobi ni mikutano kati ya makundi ya wapiganaji na wafuasi wake, ikilenga kuanzisha serikali nyingine tofauti na serikali halali iliyopo sasa.
Wizara hiyo imelaumu uamuzi wa serikali ya Kenya wa kuitisha mkutano huo, ikisema kuwa ni ukiukaji wa mamlaka halali na usalama wa taifa la Sudan.
Pia imeonya kuwa hatua hiyo inaleta tishio kubwa kwa amani na usalama wa kikanda, na kwa uhusiano imara wa ujirani mwema kati ya nchi za kanda hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma