

Lugha Nyingine
Mbegu za nyasi kutoka Mwezini kuchipuka Duniani
Mfugaji akiendesha trekta yake iliyopakiwa nyasi za malisho ya mifugo zilizovunwa katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, Xinjiang, China, Agosti 27, 2023. (Xinhua/Hu Huhu)
Wafugaji katika Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauygur wa Xinjiang, China wanaweza kupata fursa ya kulisha ng'ombe na kondoo wao kwa nyasi za malisho kutoka nje ya dunia, kwani kundi la aina mpya za nyasi zitaanza kupandwa na kukuzwa kutoka kwenye mbegu zilizoweza kustawi baada ya safari ya kuzitoa mwezini.
Pakiti nne za sampuli za mbegu za nyasi, zenye uzito wa gramu 200 na zenye asili ya eneo la kaskazini-magharibi mwa China, zilibebwa ndani ya chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-6, ambacho kilirushwa upande wa mbali wa mwezi ambao hapo awali haukuwa umechunguzwa, mnamo Mei mwaka jana, na kurejea duniani mwishoni mwa Juni.
Taasisi ya Sayansi ya Wanyama ya Xinjiang imesema, upandaji wa majaribio wa mbegu hizo utaanza mapema Machi mwaka huu.
Wanasayansi wanasema kuwa mbegu hizo, ambazo zimeathiriwa na mazingira ya anga ya juu, zitapata mabadiliko ya vinasaba ambayo huenda yakazalisha aina bora zaidi za malisho duniani.
Mbegu hizo za kuzalishwa mwezini, ambazo kwa kawaida hupatikana Xinjiang, zinajumuisha spishi kama vile camel thorn na alfalfa.
Kwa mujibu wa Zheng Wenxin, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Xinjiang ambaye pia ni mtafiti kiongozi wa utafiti huo, mbegu hizo zinaonyesha uhimilivu mkubwa kwa udongo wenye hali ya chumvi na alkali, baridi, na ukame.
Amesema, baadhi spishi hizo zina thamani ya juu ya lishe na uwezo mkubwa wa kustahimili mazingira magumu, zikitoa mchango muhimu katika kuzuia uharibifu wa nyasi, pamoja na kupambana na hali ya ueneaji wa chumvi na jangwa katika maeneo kame ya kilimo.
Picha hii iliyopigwa na kutumwa kiotomatiki duniani na kifaa kidogo cha uchunguzi kilichotolewa kutoka muunganiko wa vifaa vya kutua-kuruka vya Chang’e-6 ikionesha mwonekano wa muunganiko wake chenyewe kwenye mazingira ya mwezini, Juni 3, 2024. (Shirika la Anga ya Juu la China/kupitia Xinhua)
Picha hii ikionesha miche ya pilipili kwenye kituo cha uzalishanaji na ukuzaji wa kisayansi wa pilipili zenye mabadiliko kutoka anga ya juu cha Zhangshugang Mjini Yueyang, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Wang Jingqiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma