

Lugha Nyingine
China yazindua modeli yake ya kwanza ya AI ya kuthibitisha magonjwa ya nadra
Mtembeleaji akijaribu roboti ya upasuaji kwenye banda la maonesho ya Kampuni ya Medtronic katika Eneo la Maonyesho ya Vifaa Tiba na Bidhaa za Huduma za Afya kwenye Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 5, 2024. (Xinhua/Zhang Cheng)
BEIJING - China imezindua modeli kubwa ya AI ambayo kwa sekunde chache tu inaweza kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa uwepo wa hali ya nadra ya kinasaba isiyo ya kawaida, kama vile ugonjwa wa Rett au ugonjwa wa Angelman, au hali ya utatanishi ya uundaji wa neva mwilini, ikiwa pamoja na mapendekezo ya matibabu, idara maalum za kutoa ushauri na kufanya vipimo hitajika.
Modeli hiyo inaweza kufanya kazi mara tu yameingizwa maelezo ya dalili kama vile "utambuzi wa kuchelewa kidhahiri kwa ukuaji wa mtoto katika kutembea, kuongea, na kufanya mawasiliano na jamii tangu alipokuwa na umri wa miaka miwili" kwenye sehemu yake ya mazungumzo.
Hali hiyo imejitokeza wakati wa majaribio ya modeli hiyo, PUMCH-GENESIS, ambayo inatumika maalumu katika kuthibitisha magonjwa ya nadra. Iliundwa kwa pamoja na Hospitali ya Beijing Xiehe (PUMCH) na Idara ya utafiti wa Otomesheni ya Taasisi kuu ya Sayansi ya China.
Hospitali hiyo imesema kwamba majaribio ya kazi ya umma yameanza hivi karibuni juu ya uwezo wa modeli hiyo katika kukamilisha uthibitishaji na ushauri wa hatua ya kwanza, pamoja na uwekaji wa miadi.
Ingawa magonjwa ya nadra hayaonekani mara kwa mara, lakini kutofautisha magonjwa hayo yenye hali nyingi mbalimbali kumesababisha vizuizi vikubwa kwa kazi ya uthibitishaji sahihi.
Kuthibitisha kwa makosa na kuahirishwa kwa utambuzi wa magonjwa hayo ya nadra bado ni changamoto kubwa kwa wagonjwa, na modeli ya AI ya PUMCH-GENESIS na vyombo vingine viko tayari kuondoa mapengo hayo ya kimfumo.
Zhang Shuyang, Mkuu wa Hospitali ya Beijing Xiehe, ameelezea kuwa kuundwa kwa vyombo vya AI vinavyosaidia uthibitishaji wa magonjwa kumekuwa lengo la siku zote la timu ya wataalam wa hospitali hiyo kwa magonjwa ya nadra. Amesema, kwa mujibu wa msingi wa ujuzi wa magonjwa ya nadra uliokusanywa nchini China na takwimu za kinasaba kutoka kwa wakazi wake, PUMCH-GENESIS ya Hospitali ya Beijing Xiehe ni modeli ya kwanza ya kuthibitisha magonjwa ya nadra duniani iliyoundwa kutokana na umaalum wa idadi ya watu wa China kwani modeli hiyo imeongeza usahihi na ufanisi wa uthibitishaji wa madaktari, na kupunguza muda wa kuthibitshwa kwa magonjwa ya nadra.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma