

Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuzidisha ushirikiano wa pande mbili
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), katika wakati wa kufanyika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kundi la 20 (G20) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Februari 20, 2025. (Xinhua/Zhang Yudong)
JOHANNESBURG - Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Alhamisi katika wakati wa kufanyika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kundi la 20 (G20) mjini Johannesburg, akiahidi kuendeleza kwa kina ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali.
Kwenye mkutano huo, Ramaphosa amemwomba Wang kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi Jinping wa China na kutoa shukrani zake za dhati kwa China kwa uungaji mkono wake wa kithabiti kwa mapambano ya Afrika Kusini ya kupigania uhuru wa taifa na msaada wake muhimu katika kuharakisha maendeleo ya nchi hiyo.
“Afrika Kusini, ambayo inathamini hali ya kuaminiana kwenye ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili na kuichukulia China kama rafiki wa kutegemewa, itaendelea kufuata bila kuyumba sera ya kuwepo kwa China Moja,” amesema Ramaphosa.
Rais huyo ameahidi kuwa nchi yake inapenda kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kivitendo na China katika sekta mbalimbali na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Afrika Kusini na China uendelee kupata mafanikio makubwa zaidi.
Kwa upande wake, waziri Wang ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amewasilisha salamu za kikunjufu za Rais Xi kwa Rais Ramaphosa, akisema kuwa, China na Afrika Kusini siku zote zinaelewana na kuungana mkono na kufanya mawasiliano na uratibu wa karibu, jambo ambalo limeonesha kiwango cha juu cha uhusiano wa pande mbili.
“Katika kukabiliana na mabadiliko na hali ngumu ya utatanishi duniani kwa hivi sasa, China itashikilia mkazo wake wa kimkakati na kuendesha vizuri mambo yake kwa uthabiti,” amesema Wang.
Amesema kuwa China inajitahidi kufanya ujenzi wa mambo ya kisasa yenye umaalumu wa China kwa pande zote, na inapenda kushirikiana na Afrika Kusini na nchi nyingine katika kuhimiza mambo ya kisasa duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma