

Lugha Nyingine
Madaktari wa China kufanya upasuaji bila malipo kwa wagonjwa 600 wa mtoto wa jicho nchini Zimbabwe
Daktari wa China akimpima mgonjwa kwenye hospitali mjini Harare, Zimbabwe, Februari 19, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)
HARARE - Wagonjwa 600 wa mtoto wa jicho nchini Zimbabwe watafanyiwa upasuaji bila malipo kutoka kwa madaktari wa China chini ya mpango wa "Safari ya Mwanga" unaosaidiwa na China.
Madaktari 12 kutoka Hospitali ya Umma ya Mkoa wa Hunan wa China watafanya upasuaji huo kuanzia Februari 23 hadi Machi 1 mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, Hong Xiuqin, kiongozi wa timu hiyo, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua Jumatano wiki hii.
“Uchujaji wa majina ya wagonjwa stahiki ulianza Februari 12 na kwa sasa unaendelea,” Hong amesema, akiongeza kuwa timu hiyo ya madaktari ya China itashirikiana na madaktari wenyeji, kutoa mafunzo papo kwa hapo, na kushiriki katika mawasiliano ya kitaaluma na wahudumu wa afya wa Zimbabwe.
Mpango huo unaadhimisha miaka 45 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zimbabwe na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa ushirikiano wa pande mbili wa matibabu.
Hong amesema mpango huo unalenga kuhimiza ushirikiano na mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwa kuleta mwanga na matumaini kwa wagonjwa wa Zimbabwe.
"Matukio ya mtoto wa jicho nchini Zimbabwe yako juu, na tunajali kuhusu afya ya watu wa Zimbabwe," amesema, akiongeza kuwa serikali ya China inatilia maanani ushirikiano na urafiki kati ya China na Zimbabwe.
Daktari wa China akiwaonyesha wageni aina mbalimbali za dawa za jadi za China kwenye Kituo cha Tiba za Jadi za China (TCM) na Matibabu ya Acupuncture cha Zimbabwe na China mjini Harare, Zimbabwe, Desemba 2, 2024.(Xinhua/Tafara Mugwara)
Boniface Macheka, mkuu wa magonjwa ya macho katika Hospitali za Kundi la Parirenyatwa, amesifu mpango huo kama ushuhuda wa uhusiano kati ya Zimbabwe na China.
"Kuna msingi wa kihistoria kwenye uhusiano kati ya nchi yetu na China. Ninaamini uhusiano huu utaimarishwa zaidi na mpango huu," ameliambia Xinhua.
Ameelezea matumaini kwa ushirikiano zaidi kati ya pande mbili wa matibabu katika siku zijazo. “Tunatumai kuwa tutaweza kuongeza aina mbalimbali za upasuaji tunaofanya katika hospitali hii ili tuweze kuhudumia wananchi wetu vyema na kufanya huduma zipatikane zaidi,” amesema.
Mkoa huo wa Hunan umekuwa ukitekeleza miradi kadhaa ya matibabu nchini Zimbabwe kwa miaka mingi, ikiwemo ya mipango ya afya ya uzazi na mtoto, kinga na matibabu ya kichocho, na mafunzo ya dawa za jadi za China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma