Idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa nchini Madagascar yafikia 11

(CRI Online) Februari 21, 2025

Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Usimamizi wa Hatari na Majanga nchini Madagascar imesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa inayonyesha nchini humo kuanzia ijumaa wiki iliyopita imeongezeka na kufikia 11.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mvua hiyo na mafuriko yameathiri watu zaidi ya 16,000, hususan katika maeneo ya nyanda za juu katikati na kusini mashariki mwa nchi hiyo, na kusababisha watu 9,000 kuhamishiwa katika maeneo ya makazi ya muda.

Inaeleza kuwa, shule zimefungwa kwa muda katika mikoa iliyoathiriwa na mvua hiyo ikiwemo mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo na maeneo ya jirani tangu jumatatu wiki hii, na mamlaka husika zimetoa wito kwa wakazi kuwa makini endapo hali ya hewa itakuwa mbaya zaidi katika siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha