

Lugha Nyingine
Kenya kurekebisha mahitaji ya visa ili kuvutia zaidi utalii wa usafiri wa meli
(CRI Online) Februari 24, 2025
Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali ya Kenya itarekebisha mahitaji ya kuomba visa ya kawaida na Uidhinishaji wa Wasafiri Kielektroniki (eTA) kwa abiria wanaowasili katika bandari ya Mombasa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza utalii wa usafiri wa meli.
Rais Ruto amesema visa hiyo ya eTA itawezesha watalii wa kusafiri kwa meli wanaotaka kutembelea Mombasa kusafiri kwa uhuru kati ya meli na mji huo, bila kuhitaji idhini kila mara wanaposhuka kutoka kwenye meli zao.
Kwa mujibu wa Rais Ruto, mabadiliko hayo ya visa yataendana na marekebisho ya hivi karibuni yaliyofanywa kwa abiria wa kimataifa wanaowasili katika viwanja vikuu vya ndege vya Kenya, ili kuhakikisha mchakato sawa wa kuingia nchini kwa wasafiri wote.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma