

Lugha Nyingine
RSF ya Sudan na washirika wake wasaini makubaliano ya kuunda "serikali ya umoja"
Vikosi vya Mwitikio wa Haraka vya Sudan (RSF) na washirika wake, wamesaini makubaliano mjini Nairobi kwa lengo la kuanzisha serikali ya umoja katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao.
Makubaliano hayo yamesainiwa licha ya upinzani mkali kutoka kwa Baraza la Mamlaka ya Mpito ya Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al Burhan, ambaye ameielezea hatua hiyo kuwa inaweza kuyumbisha zaidi nchi hiyo.
Hatua hiyo ya watia saini, akiwemo kiongozi mashuhuri wa waasi wa kundi la RSF Bw. Abdelaziz al-Hilu, imeelezwa kuwa itafungua njia ya kuanzisha Muungano wa Waasisi wa Sudan, unaolenga kuhimiza amani na umoja katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi hao nchini Sudan.
Wakati hilo linajiri, Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kuvunja ngome ya waasi ya mji wa El Obeid Jimboni Kordofan Kaskazini na kuudhibiti tena mji wa al-Gitaina wa Jimbo la White Nile.
Msemaji wa Jeshi la serikali ya Sudan (SAF), Bw. Nabil Abdalla, amesema kwenye taarifa kuwa vikosi vya jeshi la serikali kutoka Jimbo la White Nile vimeangamiza “vikosi vya wanamgambo” na kuusafisha mji wa al-Gitaina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma