Viongozi wa Libya na Somalia wajadili ushirikiano katika uwekezaji na elimu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 25, 2025

Mwenyekiti wa Kamati ya Urais ya Libya Mohamed Menfi (Kulia) na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Libya, Februari 24, 2025. (Picha na Hamza Turkia/Xinhua)

TRIPOLI - Mwenyekiti wa Kamati ya Urais ya Libya Mohamed Menfi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Libya na Somalia kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu kufuatia mazungumzo na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliye ziarani nchini humo.

Rais Menfi amesema, nchi hizo mbili zimetia saini makubaliano kadhaa ya kumbukumbu ya ushirikiano katika uwekezaji, mafunzo, na elimu.

"Tunathibitisha uungaji mkono wetu kwa Somalia pamoja na jukumu muhimu la Somalia katika kipindi hiki na ushirikiano wetu katika majukwaa na mashirika ya kimataifa," Menfi amesema.

Amesisitiza fursa za uratibu kwa kupitia uanachama wa pamoja katika Umoja wa Nchi za Kiarabu, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Mataifa, akisema kuwa, hivi sasa Somalia ni nchi mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayowakilisha Afrika ikiwa pamoja na Algeria na Sierra Leone.

Rais Menfi ameelezea matumaini kwamba Somalia itatoa uungaji mkono kwa Libya katika ukamilifu wa ardhi yake, utulivu wake, na uchaguzi ujao wa wabunge na rais wa Libya.

Kwa upande wake Rais Mohamud amesisitiza uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili, akiahidi uungaji mkono wa Somalia kwa Libya.

Mapema ya jana Jumatatu, Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah alikutana na Rais Mohamud kujadili uhusiano wa pande mbili na masuala ya kikanda.

Pande hizo mbili zilitia saini makubaliano yakiwemo ya kusameheana viza kwa raia wa nchi hizo wenye pasi za kusafiria za kidiplomasia na makubaliano ya mashauriano ya kisiasa kati ya wizara zao za mambo ya nje.

Makubaliano mengine yanayohusu ushirikiano wa maendeleo ya miji kati ya Tripoli na Mogadishu, na mipango ya kuanzisha kamati ya pamoja ya ngazi ya juu kukagua biashara ya zamani na kujadili uwekezaji wa Libya nchini Somalia, taarifa ya serikali ya Libya kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook imeeleza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Urais ya Libya Mohamed Menfi (Kulia) na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud wakipeana mikono kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Libya, Februari 24, 2025. (Picha na Hamza Turkia/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha