Mwanariadha wa Tanzania Geay ashinda mbio za Marathon za Daegu 2025

(CRI Online) Februari 25, 2025

Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Geay ameshinda mbio za Marathon za Daegu 2025 kwa upande wa wanaume, zilizofanyika juzi Jumapili nchini Korea Kusini, akimaliza mbio hizo kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:05:20, na kumshinda Addisu Gobena wa Ethiopia kwa sekunde mbili pekee, ambaye alimaliza mbio hizo kwa muda wa 2:05:22.

Geay ambaye alikuwa mshindi wa pili wa Mbio za Marathon za Boston 2023, katika mbio hizo amemshinda mwanariadha huyo shujaa wa Ethiopia aliyeng’ara kwenye Mbio za Marathon za Dubai 2024, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Muethiopia mwingine, Dejene Magersa aliyemaliza mbio hizo kwa kukimbia kwa muda wa 2:05:59.

Mbio hizo zimeelezwa kuwa zilikuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na ushiriki wa wanariadha mashuhuri kutoka kote duniani.

Kwa upande wa Wanawake, Meseret Balete wa Ethiopia alimaliza wa kwanza kwa kukimbia mbio hizo kwa muda wa 2:24:08 huku mshindi wa medali ya dhahabu ya Michezo ya Olimpiki ya Rio De Janeiro 2016 Ruth Jebet wa Bahrain akimaliza nyuma kwa zaidi ya dakika moja na nusu kwa kutumia muda wa 2:25:43.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha