Rais wa Zimbabwe azindua eneo maalum la viwanda lililowekezwa kwa mtaji kutoka China

(CRI Online) Februari 25, 2025

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amehudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi jana Jumatatu kwa ujenzi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Nishati na Madini la Palm River linalowekezwa kwa mtaji kutoka China, akipongeza hatua hiyo kama kichocheo cha kuendeleza uchumi wa viwanda nchini Zimbabwe.

Eneo hilo lililoko katika Jimbo la Matabeleland Kusini, lenye uwekezaji wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.6 kutoka kwa kampuni ya China, litaendelezwa kwa awamu tano katika kipindi cha miaka 12.

Rais Mnangagwa amesema Zimbabwe inatarajia kuwa mradi huo utasaidia kuendeleza uchumi na kufungua fursa ambazo hazijawahi kushuhudiwa kwa ajili ya ajira na maendeleo ya kiteknolojia na kijamii.

Ameongeza kuwa mradi huo ni msukumo mkubwa katika njia ya Zimbabwe ya kuendeleza viwanda, kwani unaunganisha nishati na madini, sekta mbili muhimu zenye uwezo wa kuainisha upya mazingira ya viwanda nchini Zimbabwe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha