Waziri wa Tanzania apongeza maendeleo ya mradi wa reli ya SGR unaojengwa na China

(CRI Online) Februari 25, 2025

Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Bw. Makame Mbarawa amesema mradi wa sehemu ya tano ya reli ya SGR ya Tanzania unaojengwa na kampuni mbili za China umepata maendeleo makubwa kwa kufikia asilimia 63.04 ya ujenzi wake wote kukamilika.

Baada ya kukagua kazi ya ujenzi katika mji wa Malampaka mkoani Simiyu, Waziri Mbarawa amesema asilimia 37 iliyobaki ya mradi huo inatarajiwa kukamilika kama ilivyopangwa licha ya changamoto za ujenzi zinazoletwa na msimu wa mvua za vuli.

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa serikali ya Tanzania imedhamiria kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati, ili kuwezesha wananchi kupata huduma za reli ya kisasa zinazofanana na zile zilizopo za Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha