

Lugha Nyingine
Rais wa Botswana atoa wito kwa SADC kutafuta mustakabali wa baadaye wa nishati endelevu
Rais wa Botswana Duma Boko akihutubia ufunguzi wa Wiki ya Nishati Endelevu ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mjini Gaborone, Botswana, Februari 24, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
GABORONE - Rais wa Botswana Duma Boko akihutubia ufunguzi wa Wiki ya Nishati Endelevu ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone ametoa wito kwa nchi za Jumuiya ya SADC kuongeza uzalishaji wa nishati katika kanda hiyo na kutafuta mustakabali wa siku za baadaye wa nishati endelevu.
Boko amesema kutekeleza mikakati ya utoaji wa nishati kunahitaji juhudi zinazofanywa kwa pamoja.
"Hakuna nchi moja inayoweza kufanya hili peke yake," amesema Boko, akiongeza kuwa mustakabali endelevu wa nishati unahitaji ushirikiano wa kina kuvuka mipaka.
"Kwa kupitia kuendeleza miradi ya nishati ya kikanda, kuratibisha sera zetu na kunufaika pamoja na uzoefu mzuri zaidi, tunaweza kutumia ipasavyo zaidi rasilimali zetu za pamoja," amesema Boko.
Rais huyo amesema, nchi katika kanda hiyo nzima zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na umaskini wa nishati, zikiwaacha mamilioni ya watu kutoweza kupata huduma za kimsingi za afya, elimu na mawasiliano.
“Kuna haja ya kuboresha na kuharakisha uwezo wa kanda hiyo wa kuzalisha na kugawanya nishati za aina mbalimbali, na kutumia zaidi nishati mbadala,” amebainisha.
Chini ya kaulimbiu ya "Kuharakisha Mpango wa utatuzi wa Nishati Endelevu, Kulifanya Eneo la SADC liwe neo la nishati salama," wiki hiyo ya Nishati Endelevu ya SADC imepangwa kuendelea hadi Ijumaa, mwishoni mwa wiki hii.
Picha hii iliyopigwa Februari 24, 2025 ikionyesha ufunguzi wa Wiki ya Nishati Endelevu ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mjini Gaborone, Botswana. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma