

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wasema mapigano yameanza tena mashariki mwa DRC
UMOJA WA MATAIFA – Kuanza tena kwa mapigano katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumeua na kujeruhi raia na kuzuia shughuli za kutoa misaada, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema Jumanne.
OCHA imesema washirika wake jimboni humo wameripoti raia takribani wanne wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika mapigano hayo katika eneo la Masisi la Jimbo la Kivu Kaskazini. Pia umevuruga juhudi za kibinadamu katika eneo hilo ili kuamua aina ya misaada inayohitajika.
Hata hivyo, katika Jimbo la Kivu Kusini, viongozi jimboni humo wameripoti shule katika eneo la Kalehe, umbali wa kilomita karibu 65 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Bukavu, zinafunguliwa hatua kwa hatua. Shule katika eneo hilo zilikuwa zimefungwa wiki kadhaa zilizopita kwakuwa mapigano hayo yaliweka watoto na walimu wa shule katika hali ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Washirika wa misaada ya kibinadamu wa OCHA wameripoti kwamba silaha ambazo hazijalipuka bado ni tatizo katika maeneo mengi yaliyoathiriwa na mapigano hayo ya hivi karibuni, zikiwemo shule mbili katika mji wa Minova, umbali wa kilomita takriban 150 kaskazini mwa Bukavu.
Kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda katika wiki za hivi karibuni lilisonga mbele kuelekea kusini kutoka ngome yake ya Kivu Kaskazini, likitwaa eneo kubwa ukiwemo mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini wa Goma, katika Ziwa Kivu na kwenye mpaka na Rwanda.
Kwa upande wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, mkuu wa operesheni za kulinda amani za shirika hilo duniani, ameelezea wasiwasi wake kuhusu tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), amesema Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Akiwa ziarani nchini Sudan Kusini, Lacroix amesema MONUSCO inakabiliwa na uwezo mdogo wa kikazi katika maeneo yanayodhibitiwa na M23 lakini inaendelea kulinda raia na kupunguza ghasia katika maeneo mengine, ikilinda mamia kwa maelfu ya raia kila siku.
Lacroix amesisitiza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba hakuna suluhu ya kijeshi kwa mgogoro huo wa DRC, akibainisha kuwa kama uhasama utakoma, Umoja wa Mataifa unapenda kuunga mkono kikamilifu kusimamisha mapigano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma