

Lugha Nyingine
Jumuiya za kikanda za Afrika zateua wapatanishi wa mgogoro wa DRC
Viongozi watatu wa zamani wa nchi za Afrika wameteuliwa kuwa wawezeshaji wa utaratibu mpya wa upatanishi wa kikanda uliopangwa hivi karibuni na jumuiya mbili za kikanda, kuhusu msukosuko wa usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) zimetangaza kuwateua rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na waziri mkuu wa zamani wa Ethiopia Hailemariam Desalegn kuwa wawezeshaji wa utarabitu wao wa pamoja wa mchakato wa amani nchini DRC.
Jumuiya hizo pia zimetangaza kuitisha mkutano wa mawaziri uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu, huku zikitaka kundi la waasi la M23 ambalo limeteka miji kadhaa mikubwa mashariki mwa DRC kusitisha mapigano mara moja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma