Zambia na Tanzania zaahidi kufanya juhudi za pamoja dhidi ya uhalifu wa kimataifa

(CRI Online) Februari 26, 2025

Zambia na Tanzania zimeahidi jana Jumanne kushirikiana ili kukabiliana na tishio la uhalifu wa kimataifa.

Nchi hizo mbili zimetoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa tume ya kudumu ya pamoja uliofanyika katika mji wa kusini mwa Zambia wa Livingstone.

Mambo Hamaundu, katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Zambia, amehimiza pande hizo mbili kushirikiana ili kupambana na tishio linaloongezeka la magendo ya binadamu kwenye mipaka yao ya pamoja.

Faraji Mnyepe, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania, amesisitiza haja ya nchi hizo mbili kushirikiana kwa karibu ili kumaliza uhalifu wa kawaida mipakani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha