Marekani yawarejesha Kenya swala 17 wajulikanao kama bongo wa milimani walio Hatarini Kutoweka baada ya Miongo kadhaa

(CRI Online) Februari 26, 2025

Kenya imepiga hatua kubwa katika harakati zake za uhifadhi wa wanyamapori baada ya kurejesha nyumbani wanyamapori 17 wa milimani, jamii ndogo ya swala adimu, miongo kadhaa baada ya kupelekwa Marekani.

Wanyama hao waliokuwa hatarini kutoweka, ambao walikuwa wakiishi katika maeneo mbalimbali ya hifadhi za wanyama jimboni Florida, wamewasili nchini Kenya siku ya Jumapili usiku na kupokelewa na Waziri wa Utalii na Wanyamapori Rebecca Miano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

"Swala hawa aina ya bongo wa milimani ambao awali walipatikana nchini Kenya pekee, walipata mateso yasiyoelezeka kwa miongo kadhaa, kutoka kupoteza makazi yako, ujangili hadi magonjwa. Idadi ya swala hawa imepungua kwa viwango vya kutisha, lakini hata katika hali ya taabu na matatizo haya, hatukukubali shinikizo la kuwaacha viumbe hawa wa kushangaza, ndiyo maana jioni hii ni kubwa," amesema Miano kwenye hafla ya kupokea swala hao.

Wanyama hao sasa watapelekwa Meru, ambako watapitia kipindi cha karantini kabla ya kurejeshwa katika makazi yao ya asili katika eneo la milimani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha