

Lugha Nyingine
Afrika Kusini yapanga kuongeza idadi ya waendesha biashara ya utalii ili kuongeza utalii kutoka China na India
Waziri wa utalii wa Afrika Kusini Bibi Patricia de Lille amesema Afrika Kusini inapanga kuongeza idadi ya waendesha biashara ya utalii chini ya Mpango wa Waendeshaji Biashara ya Utalii Wanaoaminika (TTOS) kushughulikia viza kwa ajili ya watalii wa China na India.
Bibi De Lille amesema hayo kwenye maonesho ya biashara barani Afrika yaliyoanza jumatatu mjini Johannesburg.
Afrika Kusini ilianzisha mpango wa TTOS mwaka jana ili kurahisisha mchakato wa maombi ya visa na kuongeza idadi ya watalii kutoka India na China. Kundi la kwanza la waendesha biashara ya utalii 65 walioteuliwa kutoka Afrika Kusini, India, na China walianza kushughulikia maombi ya viza kupitia mpango huo kuanzia Februari 12.
“Afrika Kusini pia inafanya mazungumzo na mashirika mbalimbali ya ndege ili kuboresha usafiri wa abiria kati yake na India na China” Waziri huyo amesema, akidokeza kuwa baada ya kulegeza masharti ya viza kwa raia wa Kenya na Ghana, idadi ya watalii kutoka nchi hizo mbili imeongezeka kwa kiasi kikubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma