Kenya yazindua ununuzi wa dhamana za Euro zenye thamani ya dola milioni 901 ili kupunguza mzigo wa madeni

(CRI Online) Februari 26, 2025

Kenya imetangaza mpango wa kununua tena dhamana za Euro zenye thamani ya dola za kimarekani takriban milioni 901.8, ambayo ilikuwa sehemu ya hati fungani za Euro zenye thamani ya dola bilioni 2.1 zilizotolewa Mei 2019.

Hazina ya Taifa ya Kenya imesema mapato yanayotokana na hati fungani hizo za Euro yatatumika kulipa sehemu ya deni, na kuwa wamiliki wa dhamana hizo waliozinunua mwaka 2019 watapewa kipaumbele wakati wa ununuzi.

Hii ni mara ya pili kwa Kenya kuchukua hatua hiyo, kufuatia ofa sawa na hiyo ya mwezi Februari mwaka jana, ilipouza hati fungani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.48 na kutumia mapato hayo kulipa hati fungani za Euro miezi minne kabla ya tarehe yake ya kuiva.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha