Karakana ya Luban ya Madagascar yawezesha vijana ujuzi kwa mustakabali wa viwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2025

Wanafunzi katika taaluma ya teknolojia ya habari wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini  Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wanafunzi wa teknolojia ya habari wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

ANTANANARIVO - Kwenye karakana ya Shirika la Ujenzi wa Reli la China kusini mwa Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Nancy Ratianarinoro kwa umakini alikuwa akirekebisha sehemu ya magurudumu ya gari. Akiwa ni mhitimu wa hivi karibuni wa Karakana ya Luban ya Madagascar katika shahada ya ukarabati wa magari, anaboresha ujuzi wake kabla ya kuingia rasmi kazini.

"Vifaa hapa ni sawa na vile tulivyotumia wakati wa mafunzo, kwa hivyo ni rahisi kwetu kuendana navyo," kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema kwa kujiamini.

Katika Shule ya Ufundi ya Chuo Kikuu cha Antananarivo, Francia Rakotondraibe, mhitimu mwingine wa Karakana ya Luban, alikuwa akionyesha kwa vielelezo uendeshaji wa kifaa cha kupitisha maji na nyumatiki akiwa kama mkufunzi msaidizi.

"Hata kama mwanafunzi, nahisi mimi ni mmoja wa nguzo za biashara yao kwa sababu ninajikita katika otomesheni, na wanafunzi wachache wamekuwa na uzoefu wa kutosha kama tuliopata," amesema, akirejelea kazi yake ya sasa ya mafunzo kazini katika kampuni kubwa ya ujenzi.

Ikiwa ilianzishwa Februari 2022 kupitia ushirikiano kati ya taasisi za China na Chuo Kikuu cha Antananarivo, Karakana hiyo ya Luban nchini humo tayari imetoa mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 100 katika taaluma nne: ukarabati wa magari, umeme wa viwandani, teknolojia ya habari, na uhandisi wa mitambo.

Baada ya miaka mitatu ya mafunzo, kundi la kwanza la wanafunzi 29 limehitimu, wengi wao wamepata kazi katika kampuni kubwa, huku wengine wakichagua kuendelea na masomo.

"Wahitimu wa Karakana ya Luban wanakaribishwa sana katika soko la kazi la ndani. Hata wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu tayari wanapokea ofa za kazi," amesema Edmond Randriamora, mkuu wa Idara ya Uhandisi wa Umeme na mwalimu katika karakana hiyo.

Kwa uungaji mkono wa mfumokazi wa ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu elimu ya ufundi stadi, karakana hiyo imeanzisha msingi wa mafunzo ya ukarabati wa magari na kuyawekea madarasa kadhaa maalumu vifaa vya hali ya juu vya kufundishia.

Madagascar imekuwa ikitafuta kikamilifu mageuzi ya kiuchumi kupitia mpango wake wa kitaifa wa ustawishaji, ikiwa ni pamoja na mpango wa "Wilaya Moja Kiwanda Kimoja" kuhamasisha maendeleo ya viwanda nchini kote.

Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi wa nchi hiyo, Loulla Chaminah amesema kuanzishwa kwa Karakana hiyo ya Luban na ushirikiano wa karibu wa elimu ya ufundi stadi kati ya Madagascar na China vinaendana na mkakati mpana wa maendeleo wa taifa hilo.

Wanafunzi katika taaluma ya uhandisi wa mitambo wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini  Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wanafunzi katika taaluma ya uhandisi wa mitambo wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wanafunzi katika taaluma ya ukarabati wa magari wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini  Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wanafunzi katika taaluma ya ukarabati wa magari wakiwa katika kipindi cha masomo kwa vitendo kwenye Karakana ya Luban mjini Antananarivo, Madagascar, Februari 10, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha