UNICEF yachangia Dola za Kimarekani zaidi ya 50,000 kwa watoto walioathiriwa na mafuriko nchini Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2025

Nono Kgafela Mokoka (wa pili, kushoto), waziri wa  huduma za watoto na elimu ya msingi wa Botswana, akipokea   michango kutoka kwa Joan Matji (wa pili, kulia), mwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Botswana, kwenye hafla ya kutoa michango  huko Gaborone, Botswana, Februari 26, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Nono Kgafela Mokoka (wa pili, kushoto), waziri wa huduma za watoto na elimu ya msingi wa Botswana, akipokea michango kutoka kwa Joan Matji (wa pili, kulia), mwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Botswana, kwenye hafla ya kutoa michango huko Gaborone, Botswana, Februari 26, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE – Shirika la Mfuko wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetoa pula 700,000 (dola za Kimarekani karibu 50,772) katika msaada wa dharura kwa Wizara ya Huduma za Watoto na Elimu ya Msingi ya Botswana kusaidia watoto walioko katika mazingira magumu ambao waliathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni.

“Shirika la Umoja wa Mataifa limesikiliza ombi la serikali la kuendeleza uingiliaji kwa suala la watoto na kukabiliana na mafuriko,” amesema Joan Matji, mwakilishi wa UNICEF nchini Botswana, kwenye hafla ya kutoa misaada iliyofanyika jana Jumatano huko Gaborone, Botswana.

Kwa ushirikiano na Chama cha Msalaba Mwekundu cha Botswana, shirika hilo litatoa misaada ya dharura na kufanya juhudi za ukarabati wa muda wa kati katika jamii zilizoathiriwa na mafuriko, likihakikisha jamii hizo zinapata huduma za kimsingi na uungaji mkono wa usafi vilevile ulinzi wa watu walio hatarini.

"Tutashirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu cha Botswana katika kusambaza vitu vya mahitaji ya kimsingi, vifaa vya usafi, maji salama ya kunywa katika maeneo yaliyoathirika, maji chumvi ya kunywa ili kurejesha maji mwilini, pamoja na kufanya mawasiliano na vituo vya afya ili kuchukua hatua za ulinzi wa watoto katika vituo vya uokoaji," amesema Matji.

Nono Kgafela Mokoka, waziri wa huduma za watoto na elimu ya msingi wa Botswana, amesema michango hiyo itasafirishwa kuelekea kusaidia watoto takriban wote walioathiriwa na mafuriko, hasa wale walio katika maeneo ya mbali, na kuharakisha usambazaji wa vitu vya mahitaji ya kimsingi katika maeneo hayo yaliyoathirika.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya kitaifa ya usimamizi wa maafa ya Botswana imeeleza kuwa, kaya jumla ya 2249, wakiwemo watu 6423, watoto 2631, na wazee 561 wameathirika, . 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha