Kongamano la China na Afrika lililofanyika Cairo lasisitiza ushirikiano na uhusiano wa kitaaluma

(CRI Online) Februari 27, 2025

Mhadhara wa 22 wa China uliofanyika mjini Cairo umewaleta pamoja wataalam na maofisa zaidi ya 200 kutoka China na Misri, kujadili kuongezeka kwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa Nchi za Kusini.

Kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya China-Afrika na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Mfereji Suez cha Misri, likiwa na kaulimbinu “Kuongeza Ushirikiano kati ya China na Afrika ili Kuchochea Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa Nchi za Kusini”, limejikita katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya China na Misri, kupanua mabadilishano ya kitaaluma, na kuongeza uungaji mkono wa kiweledi kwa juhudi za ujenzi wa mambo ya kisasa za nchi zinazoendelea.

Majadiliano kwenye kongamano hilo yamesisitiza kuboresha ubora na ufanisi wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mazingira ya kimataifa yanayobadilika kwa kasi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha