Maofisa kwenye mpaka wa Ethiopia-Kenya waahidi kushughulikia migogoro kati ya jamii

(CRI Online) Februari 27, 2025

Maofisa wa usalama kutoka Ethiopia na Kenya wamesisitiza tena ahadi yao ya kushughulikia migogoro kati ya jamii ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara na kujenga amani ya kudumu katika eneo hilo la mpakani.

Taarifa kutoka serikali ya wilaya ya Dasenech ya Ethiopia, imesema ahadi hiyo imetolewa baada ya maofisa waandamizi wa eneo la kusini mwa Ethiopia na kaunti ya Turkana ya Kenya kukutana Jumanne wiki hii, kujadili hali ya usalama mpakani kufuatia mapigano makali kutokea hivi karibuni katika eneo la Todonyang, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 33 kutoka pande zote mbili.

Maofisa hao wamesisitiza haja ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hiyo ya kiusalama kupitia kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya jamii jirani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha