

Lugha Nyingine
Ndege ya kijeshi ya Sudan yaanguka kaskazini mwa Khartoum, na kusababisha vifo
Ndege ya kijeshi ya Sudan imeanguka Jumanne katika mji wa Omdurman, kaskazini mwa Khartoum, na kusababisha vifo vya wahudumu wa ndege na maafisa kadhaa wa jeshi la Sudan.
Jeshi la Sudan limesema katika taarifa kuwa, ndege hiyo ya aina ya Antonov iliyoanguka ilikuwa ikipaa kutoka Kambi ya Kijeshi ya Wadi Seidna, umbali wa kilomita takriban 22 kaskazini mwa Khartoum, na ilianguka muda mfupi baada ya kupaa.
Chanzo cha habari ambaye ni mwanajeshi, asiyetaka kutajwa jina, aliliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa, ndege hiyo ya Antonov ilianguka katika wilaya ya Al-Hara 76, kutokana na tatizo la kiufundi.
Ndege hiyo ilikuwa inatekeleza operesheni ya kijeshi, ikiwa imebeba maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa kijeshi pamoja na wakandarasi wanne.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma