Polisi zaidi ya 600 wa DRC warejeshwa kutoka Burundi

(CRI Online) Februari 27, 2025

Serikali ya Burundi imesema polisi zaidi ya 600 na askari 28 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) waliotafuta hifadhi nchini Burundi hivi karibuni wamerejeshwa nchini mwao usiku wa Jumatatu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma ya Burundi, Pierre Nkurikiye amesema Jumanne kuwa, polisi 612 walioingia Burundi kupitia kituo cha mpaka cha Gatumba kilichoko Mutimbuzi mkoani Bujumbura na askari 28 walioingia Burundi kupitia mkoa wa Cibitoke wamerejeshwa nchini mwao.

Amebainisha kuwa polisi na askari wote wamerejea nyumbani “kwa hiari”, na kukaribishwa nyumbani DRC na naibu gavana wa Jimbo la Kivu Kusini kwenye kituo cha mpakani cha Gatumba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha