Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Afrika wapanga mikakati ya kutuma vikosi nchini Somalia

(CRI Online) Februari 28, 2025

Mawaziri wa ulinzi wa nchi mbalimbali za Afrika wamemaliza mkutano wa siku mbili uliojikita katika kuthibitisha idadi ya wanajeshi kwa ajili ya misheni mpya ya kulinda amani nchini Somalia, iliyoanza kazi mwezi Januari mwaka huu.

Mkutano huo wa mawaziri wa Kamati ya Uratibu wa Operesheni za Somalia (SOCC), uliomalizika Jumatano wiki hii umeazimia kuitisha mkutano wa wataalamu wa kiufundi ili kukamilisha mpango huo wa kutuma wanajeshi watakaojiunga na ujumbe wa Umoja wa Afrika wa kuleta utulivu na uungaji mkono nchini Somalia (AUSSOM).

Vyanzo vya habari vinasema, mawaziri hao wamekubaliana kuwa ujumbe huo unatakiwa kujumuisha wafanyakazi 11,900 wakiwemo wanajeshi, askari polisi, na wafanyakazi wa kiraia wa kutoa uungaji mkono.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha